Fahari Kuku Farm (FKF) ni kampuni ya kuzalisha na kusambaza vifaranga bora wa kuku chotara iliyopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Pia tunazalisha na kusambaza chakula cha vifaranga na kuku wakubwa

Tumewekeza katika kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora zinazokidhi mahitaji halisi ya wafugaji wadogo wanaohitaji kufanya ufugaji wenye tija kiuchumi. Wateja wetu ni wafugaji na wajasilaimali kutoka Mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Singida, Simiyu, Katavi, Kigoma na Kagera

Tuna taaluma na uzoevu wa zaidi ya miaka sita katika uzalishaji na usambazaji wa vifaranga na chakula cha kuku. Tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji pia tunatengeneza na kuuza mashine za kuzalisha vifaranga (incubators) za ukubwa mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji

Tupo Kahama, eneo ni Lugela maarufu kibao cha nyakanazi

Karibu ungana nasi katika safari ya ufugaji wenye tija